Uchaguzi wa viongozi mbalimbali unaendelea nchini Tanzania licha ya matatizo mengi yanayokabili shughuli hiyo.
Katika maeneo mengi yanayoegemea mrengo wa upinzani, majina ya wengi waliojisajili kielektroniki kupiga kura yanakosekana katika karatasi zilizobandikwa ukutani.
Akizungumza muda mchache uliopita kupitia mtandao wake wa Facebook, mwanahabari huru na mwimbaji wa nyimbo za injili Faustine Munishi ameelezea kukerwa kwake na shughuli hiyo.
Munishi amesema ilimbidi kusafiri hadi kituo cha nne kupiga kura licha ya kuwahi mapema. Jina lake halikuwa katika kituo alichojisajili.
Katika kisiwa cha Zanzibar, hali pia ni vilevile. Vita vimeibuka katika maeneo mbalimbali huku wengi wakisusia shuguli hiyo.
Je, inawezekana hii inadhihirisha njama ya serikali tawala ya Rais John Pombe Magufuli kuiba na kusalia madarakani? Tusubiri tuone.
Reporter and Editor working side-by-side with teams in the field to shape, write and produce unique and dynamic stories for Silvan News’ TV, website and social platforms.